Proverbs 7:5-27

5 awatakuepusha na mwanamke mzinzi,
kutokana na mwanamke mpotovu
na maneno yake ya kubembeleza.

6Kwenye dirisha la nyumba yangu
nilitazama nje kupitia upenyo
kwenye mwimo wa dirisha.
7 bNiliona miongoni mwa wajinga,
nikagundua miongoni mwa wanaume vijana,
kijana asiye na akili.
8Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake,
akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke
9 cwakati wa machweo, jua likipungua nuru yake,
giza la usiku lilipokuwa likiingia.

10 dNdipo huyo mwanamke akatoka kumlaki,
hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.
11 e(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi,
miguu yake haitulii nyumbani;
12 fmara kwenye barabara za mji,
mara kwenye viwanja vikubwa,
kwenye kila pembe huvizia.)
13 gHuyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu,
na kwa uso usio na haya akamwambia:

14 h“Nina sadaka za amani nyumbani;
leo nimetimiza nadhiri zangu.
15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki;
nimekutafuta na nimekupata!
16 iNimetandika kitanda changu
kwa kitani za rangi kutoka Misri.
17 jNimetia manukato kitanda changu
kwa manemane, udi na mdalasini.
18 kNjoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi;
tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!
19Mume wangu hayupo nyumbani;
amekwenda safari ya mbali.
20Amechukua mkoba uliojazwa fedha
na hatakuwepo nyumbani karibuni.”

21 lKwa maneno laini yule mwanamke akampotosha;
alimshawishi kwa maneno yake laini.
22 mMara huyo kijana alimfuata yule mwanamke
kama fahali aendaye machinjoni,
kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,
23 nmpaka mshale umchome ini lake,
kama ndege anayenaswa kwenye mtego,
bila kujua itamgharimu maisha yake.

24 oSasa basi wanangu, nisikilizeni;
sikilizeni kwa makini nisemalo.
25 pUsiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke,
wala usitangetange katika mapito yake.
26 qAliowaangusha ni wengi;
aliowachinja ni kundi kubwa.
27 rNyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini,
Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.
Copyright information for SwhNEN